Nov 3, 2021

Mwanasheria wa Tigo atoa ushahidi kesi ya Freeman Mbowe na Wenzake

Fredy Kipara (38) ambaye ni Shahidi wa tano upande wa Jamhuri katika kesi ya uhujumu uchumi yenye mashtaka ya ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake, ametoa taarifa za miamala ya fedha aliyoifanya Mbowe kwa nyakati tofauti.
Kwa mujibu wa Kipara, Mbowe alifanya miamaka mbalimbali kutoka kwenye simu yake ya tigo kwenda kwa mtu mwingine kiasi cha Sh.500,000.

Kapara ambaye ni mwanasheria wa Kampuni ya mtandao wa simu ya Tigo, aliyeajiriwa mwaka 2012 kitengo cha sheria, ametoa ushahidi wake jana  Jumanne, tarehe 2 Novemba 2021, katika Mahakama Kuu, Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, Dar es Salaam.

Ametoa ushahidi huo akiongozwa na Wakili wa Serikali, Nasorro Katuga ambaye amemuuliza majukumu yake ya kila siku ni yapi na kujibu ni, kushauri viongozi maswala yanayohusu sheria, kutengeneza, kusoma, kupitia na kusaini mikataba.

Pia amesema kufuatilia, kusimamia kesi zote zinazohusiana na tigo kumsaidia vyombo vya ulinzi na usalama katika kupata taarifa mbalimbali kutoka kwa wateja zinapohitajika.

Kipara amesema, miongoni mwa vyombo vya usalama wanavyovisaidia kupata taarifa baada ya kuziomba kwa njia rasmi ya maandishi ni Polisi, Jeshi, Anga kama ni Ardhi na vyombo vyote vinavyofanya uchunguzi wa kisayansi.

Amedai taarifa zozote ambazo zitakuwa zinahitajika wao wanazo, kuna kupiga na kupokea simu za wateja wetu zinaitwa Call Details, taarifa za miamala ya fedha na kutuma na kupokea fedha

Pia, kuna Recharge ya vocha na kutumia pamoja na matumizi yake, taarifa za usajili na taarifa nyingine zote zinazoambatana kama Nida, locations na bill mbalimbali anazolipa.

Alipoulizwa hizo taarifa anazitoa wapi, shahidi amesema taarifa zote za kampuni pamoja na wateja wake zinakuwa stored kwenye Server ambayo inakuwa na ulinzi ili isiingiliwe na wana mitandao.

Mbali na Mbowe kwenye kesi hiyo wengine ni, Adam Kasekwa, Mohamed Abdillah Ling’wenya na Halfan Hassan Bwire, waliokuwa makomandoo wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ). Kwa pamoja wanatuhumiwa kupanga vitendo vya kigaidi.

Mahojiano baina ya mwanasheria wa Tigo na wakili wa serikali yalikuwa hivi;

Shahidi: Tigo- taarifa zote zinakuwa Served Automatically mtu anapo piga simu mnara unasoma na taarifa zinashuka na zina switch na kwenda Automatically kwenda kwenye server kuwa stored

Wakili wa Serikali: Ishu ya kuvisaidia vyombo vya Ulinzi na usalama utaratibu ukoje

Shahidi: Kila chombo cha ulinzi kinahitaji kuwa na hizo document iwe amri au ombi lazima iwe In writing

Wakili wa Serikali: In Writing unamaanisha nini

Shahidi: Iwe na Proper heading, Iwe na Nini wanataka

Wakili wa Serikali: Kwa hiyo ni barua lazima iwe hivyo

Shahidi: Ni barua au order ya Mahakama

Wakili wa Serikali: Kwa kumbukumbu zako Mnamo tarehe 02 Julai 2021 ulikuwa wapi

Shahidi: Nilipata barua mbalimbali za maombi, katika barua hizo kuna barua ilitoka  kwa kamishina wa upelelezi wa kisayansi ikihitaji taarifa za namba ya mteja

Wakili wa Serikali: Ulisema kuna aina mbili za maombi kuwa kuna maombi na amri Je, hiyo ilikuwa nini

Shahidi: Ilikuwa ni Requeast

Wakili wa Serikali: Unaweza kukumbuka ilikuja kwa maombi ya kuomba taarifa fulani za namba fulani Je, unaweza kukumbuka? Hiyo namba uliyoombewa kwenye Hiyo barua

Shahidi: Baada ya kuifikiria anaitaja 0719933386

Wakili wa Serikali: Hilo ombi lilikuwa ni maombi mangapi

Shahidi: Yalikuwa maombi ya miamala ya fedha na usajili.

Wakili wa Serikali: Baada ya kupokea sasa, nini ulifanya kuhusiana na ombi hilo

Shahidi: Nilipopokea ombi kutoka kwa kamishina, niliingia kwenye kompyuta yangu, nikaweka Credentials zangu, nikafunga screen server, nikaingiza namba ya simu kwenye procedure ambayo inaniruhusu kupata Tigo Pesa

Wakili wa Serikali: Unakumbuka ilikuwa ni yawakati gani

Shahidi: Walitaka taarifa za miamala ya fedha kutoka 01 June ya 2020 mpaka 31 June ya 2020. Nikaingia kwenye kompyuta nikaziona na kuzi print kisha nikaingia namba kuona taarifa za usajili.

Wakili wa Serikali: Kwenye namba uliyotaja baada ya kuprint ukafanya nini

Shahidi: Niliandika barua kumjibu kamishina wa makosa ya kisayansi alichokuwa anakitafuta nikamrudishia. Katika barua nilisha print lazima nigonge muhuri na signature yangu na lazima muhuri wa MIC Tanzania Ltd

Wakili wa Serikali: Ukiambatanisha na nini hiyo barua

Shahidi: Cover letter, barua ya kamishina, miamala ya kifedha na usajili.

Wakili wa Serikali: Shahidi tufafanulie Maneno kama sender maana yake nini

Shahidi: Send My Op namba 0719933386 Receiver 0787555200, Muamala wa tarehe 20 Julai 2020 Sh.500,0000 saa 2:21 na salio ilikuwa Sh. 2.3 milioni

Wakili wa Serikali: Twende kwenye hii ya usajili

Shahidi: Imeanza na namba pale juu. Jina la kwanza jina la katika, Taifa, jenda na vitu vinginevyo. Mstari unaofuata 0719933386 Jina Freeman Last name Mbowe

Wakili wa Serikali: Tarehe 20 Julai 2020 inaonekana nini

Shahidi: Kuna namba ya Tigo ya 0719933386 imetuma kiasi cha fedha laki tano kwenda kwa namba ya Airtel namba 0787555200

Credit: Mwanahalisi

Feb 20, 2018

VIDEO: Baba wa Akwilina atamani kukutana na muuaji wa mwanaye amng'ate hata meno hadi afe

Akwilini Shirima ambaye ni baba mzazi wa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwiline aliyepigwa risasi na polisi Februari 16, 2018 amesema siku akikutana na askari aliyemuua mwanaye atapambana naye.

Akizungumza leo Februari 19, 2018 nyumbani kwake Kijiji cha Olele, Shirima alisema endapo muuaji atakuwa ni kijana mwenye nguvu kumzidi, atapambana naye hata kwa kumuuma kwa meno.
"Najua ni ngumu kukutana na aliyempiga mwanangu risasi, lakini laiti ningekutana naye kama ni kijana mwenye nguvu kunizidi nitapambana naye hata kumuuma kwa meno,” amesema.
“Kama ni mzee mwenzangu nitapambana naye hadi kifo ila kwa bahati mbaya siwezi kumpata, hivyo sina namna. Kwa kweli hiki kifo kimezima ndoto ya familia ya kuondokana na umasikini.”


Shirima ameiomba Serikali kuliangalia suala hilo kwa kina na kuona namna ya kumsaidia kwa kuwa tegemeo lake limeondoka na wao kwa sasa hawana msaada wowote na wanachosubiri ni kifo.
"Jamani hii ni taa yangu imezimika na kuniacha gizani kwani toka nimepata taarifa za kifo chake sijaweza kula chochote. Nimekuwa kama nguruwe aliyetelekezwa porini bila msaada," amesema.
"Nilipopata taarifa za kifo cha mwanangu nilishtuka sana na kuhoji ni mwizi au nini kimetokea. Imenitia uchungu sana na siwezi hata kula"

Shirima amesema ni afadhali mwanaye angeugua akamuuguza kuliko kifo cha ghafla alichokipata ambacho kimewaacha kwenye hali ambayo haitafutika mioyoni mwao katika maisha yao yote.
Mama wa marehemu, Costanzia Akwilini amesema mauaji ya mwanaye ni ya kinyama na bora angekuwa mbuzi angekula nyama kujifariji kuliko kwa mwanaye ambaye hakuna anayeweza kumfuta machozi.
"Mwanangu hakuwa mwanasiasa ameuawa akiwa kwenye gari akielekea kwenye shughuli zake, familia tulijinyima tukajichanga kwa kushirikiana na majirani ili asome aje atukomboe,” amesema.
“Leo nasubiria niletewe maiti kwenye jeneza. Kwa kweli imeniuma sana na kunikatisha tamaa. Naomba Serikali itende haki katika tukio hili," amesema mama wa marehemu katika mahojiano hayo.

Akwilina alifariki dunia Februari 16, 2018 baada ya kupigwa risasi kichwani akiwa kwenye daladala wakati polisi wakiwatawanya waandamanaji ambao ni wafuasi wa Chadema.

Feb 16, 2018

Baraza la Watu Wanaoishi na UKIMWI Lataka Itungwe Sheria Bungeni Kuwalazimisha Watu Kupima VVU

Baraza la watu watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi, Katika halmashauri ya Wilaya ya Mbozi Mkoa wa Songwe wameliomba Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kutunga Sheria itakayopelekea watu kupima Ukimwi kwa lazima.

Hayo yamesemwa na watu wanaoishi na Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi Konga ya Mbozi wakati walipotembelewa na Kamati ya Bunge ya Ukimwi ambayo ipo ziarani mkoani humo.

Wamesema  kuwa hatua hiyo itasaidia kwenye Mapambano ya Maambukizi na kuenea kwa ugonjwa huo ili kutimiza azma ya serikali ya 0.0.0 kuhakikisha kuwa ifikapo mwaka 2030 hakuna Maambukizi Mapya ya Ukimwi.

Mmoja wa Waathirika hao Stephan Jonas alisema njia ya Mbadada ya kukabiliana na Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi ni kuweka sheria ya kulazimisha kila kaya kupima ugonjwa huo.

"hili  suala inatakiwa liwe la lazima kwa sababu watu hawapimi, wanashindwa kujitambua hivyo wanaendelea kueneza kwa wengine sheria ikiwepo kila mtu apime kwa lazima itasaidia sana," alisema 

Makamu Mwenyekiti wa kamati ya Bunge, Dr Jasmini Bunga alikubalina na Ombi hilo na kueleza kuwa litasaidia mkakati wa serikali wa kukabiliana na Maambukizi mapya ya Ukimwi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la JSI linashughulika na Mifumo ya maisha na Ustawi wa  Jamii Dr. Tulia Tuhuma alisema shirika lake litaendelea kufuatilia maendeleo ya Konga (Vikundi vya watu wanaoishi na Virusi vya ukimwi) pamoja na kusaidia utoaji wa huduma ya Ukimwi.

SERIKALI YA TANZANIA YAIPIGA MARUFUKU KENYA KUINGIZA MAKONTENA ZANZIBAR KUTOKEA BANDARI YA MOMBASA

[​IMG]

Serikali ya Tanzania imezuia usafirishaji wa Makontena kwenda Zanzibar kupitia Bandari ya Mombasa Kenya.
Julius Musyoki (Kamishna wa forodha na uthibiti mipakani wa Kenya) amesema kuwa TRA wamewaandikia Kenya, wamesema katika uongezekaji wa kuingizwa kwa bidhaa kimagendo Tanzania, chanzo chake kimeonekana ni Makontena yanayoingia kupitia bandari ya Mombasa

Makontena 264 ambayo yalikuwa yaende Zanzibar yamezuiwa nchini Kenya katika bandari hiyo ya Mombasa

Makontena kadhaa yalikuwa yanapelekwa bandari ya Mombasa halafu yanasafirishwa kwenda sehemu husika kama Zanzibar kwa kupitia boti

========



Clearing agents in Mombasa could be forced to lay off employees after a ban on trans-shipment cargo to Zanzibar by the Tanzania government.

The Tanzania Revenue Authority (TRA) has written to Kenya about the decision.

A spot check revealed 264 containers destined for Zanzibar being held at the port of Mombasa.

Traders who did not wish not to be named Thursday because of the sensitive nature of the matter said TRA had given them a window only to clear the containers already in Mombasa, but the ban was still in force.

The matter first emerged during an assessment on institutions, installations and facilities of the East African Community along the northern corridor at Kenya Ports Authority headquarters in Mombasa by the team leader of the East African Legislative Assembly (EALA) delegation, Kasamba Mathias.

Trans-shipments involve cargo brought to the Mombasa port and transferred to final destinations such as the Zanzibar islands using smaller vessels such as boats.

In a notice, Kenya’s Commissioner of Customs and Border Control Julius Musyoki said TRA had reported increased cases of smuggling that adversely affected Pemba and Unguja islands.

He said the source of goods being smuggled into Tanzania had been traced to containers stripped at the Mombasa port.


credit: jamii forums

Aug 23, 2016

news alert: askari polisi watatu wauwawa, silaha yaporwa na majambazi tawi la CRDB Mbande leo jioni

Habari zilizotufikia zinasema askari polisi watatu wameuwawa katika uvamizi wa majambazi katika Benki ya CRDB tawi la Mbande jijini Dar es salam mnamo saa moja na nusu jioni ya leo Jumanne Agosti 23, 2016.

Askari waliouwawa inasemekana ni E5761 CPL YAHAYA, F4660 CPL HATIBU NA G9544 PC TTITO.

Habari zinasema majambazi hayo yamepora SMG moja kabla ya kutokomea, na kwamba tukio hili limetokea wakati askari wakibadilishana lindo. 

Mmoja wa askari waliouwawa alikuwa anaingia, mmoja alikuwa anatoka na mwingine alikuwa dereva. Inasemekana Majambazi  hayo ambayo idadi yao haijajulikana hayakuingia ndani ya bank. 

Jul 15, 2016

Breaking News: Matokeo ya Kidato cha Sita 2016 Yametoka....Bofya hapa Kuyaangalia

Matokeo  ya  Kidato  cha  Sita  2016  Yametoka....Bofya  hapo chini  Kuyaangalia

Jun 15, 2016

KAMA ULIKOSA VIDEO YA MAALIM SEIF KATIKA MKUTANO WA (CSIS) JIJINI WASHINGTON DC NIMEKUSOGEZEA HAPA





PLAY VIDEO HAPA CHINI

VIDEO: HAYA NDIYO MAJIBU YA MAALIM SEIF KUHUSU KUMPOKEA LIPUMBA ALIPOKUWA AKIHOJIWA NA VOICE OF AMERICA



play video hapa chini

Siendi tena Afrika Kusini kushoot video – Adam Juma

imageRich Mavoko, Ommy Dimpoz, Cpwaa, Q-Chief, Chege na Temba ni miongoni mwa wasanii waliowahi kusafiri na muongozaji wa video, Adam Juma kwenda kufanya video zao Afrika Kusini.
Na sasa huenda ndoto ya wasanii wengine wenye nia ya kukwea pia na AJ ili kufanya video zao bondeni huenda zikawa zimefutika rasmi.  Ni kwasababu muongozaji huyo amesema kwa sasa (walau kwa sasa) hana mpango tena wa kwenda kufanya video zake nchini humo.
“Yaani sasa hivi mtu akiniambia anataka kwenda kushoot video South Africa siendi tena,” Adam alikiambia kipindi cha Super Mega cha Kings FM ya Njombe kinachoendeshwa na Divine Kweka.
“Siwezi kwenda, sasa hivi nina commitment, watoto wanataka kwenda shule. Unalipwa hela ile ile kazi ambayo unaifanya hapa kwa siku moja, it doesn’t make any sense,” aliongeza.
“Mimi nimefanya video nyingi South Africa, lakini nimefanya kwasababu ya kuinvest, lakini sasa ukija kuangalia kwa faida kitu gani tunapata?”
AJ ameendelea kusisitiza kuwa uongozaji wa video kwa Tanzania bado haulipi na hiyo ni sababu iliyomfanya aache kufanya kazi nyingi kama zamani. Amesema kwa sasa atafanya kazi na wasanii ambao wako tayari kumlipa vile anavyotaka au mahitaji muhimu yanayohitajika kufanikisha wazo la video husika.
Hivi karibuni waongozaji wengine wa video nchini wameanzisha utaratibu wa kwenda na wasanii kufanya video Afrika Kusini. Mfano ni video ya Chafu Pozi ya Bill Nass na Pesa ya Madafu ya Jay Moe ambazo zote zilifanyika SA na kuongozwa na Msafiri wa Kwetu Studios.
Waongozaji wanadai kuwa sababu kubwa inayowapeleka Afrika Kusini kufanya video ni upatikanaji rahisi wa location ambapo kwa Tanzania huwawia vigumu kutokana na kutokuwepo utaratibu maalum na huku mamlaka zingine zikiwa na mchakato mrefu wa kuruhusu kutumiwa kwa maeneo husika.

Jenerali Ulimwengu Ataka Kikwete Ashitakiwe.....Adai Kaisababishia Serikali Hasara Kubwa

Mwanahabari nguli nchini Jenerali Ulimwengu amesema Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete anapaswa kushtakiwa mahakamani kwa kuisababishia hasara Serikali kutokana na mabilioni ya shilingi yaliyotumika katika mchakato wa Katiba ambayo haikupatikana.

Akizungumza katika tamasha la nane la Kigoda cha Mwalimu Nyerere katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) jana, Jenerali Ulimwengu alisema fedha nyingi zimepotea wakati wa kuunda Katiba Mpya ambayo haikupatikana. 

Mbali ya fedha zilizotumika na Tume ya Mabadiliko ya Katiba wakati wa kukusanya maoni na nyingine zilizotumika kurekebisha ukumbi wa Bunge uweze kubeba wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, jumla ya Sh24.53 bilioni zilitumika kulipa posho za wajumbe. 

Tamasha hilo lililojikita kujadili falsafa za Mwalimu Nyerere katika muktadha wa “Visheni ya Maendeleo ya Watu,” liliwakutanisha wasomi mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi, wanafunzi na wanasiasa wakiwamo Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Waziri mkuu mstaafu, Jaji Joseph Warioba. 

Jenerali aliyekuwa anajadili hotuba ya mgeni rasmi, Benjamin Mkapa, alisema fedha nyingi ziligharamia mchakato wa Katiba uliokuwa unaendeshwa na Tume ya Katiba chini ya Jaji Joseph Warioba, lakini ulikwama, ndiyo maana hadi leo hakuna Katiba mpya. 

“Itabidi (Kigoda cha Mwalimu) mumuite mwaka ujao, aje aeleze fedha za wananchi zilizotumika katika mchakato ule zilikuwa na sababu gani,”alisema Jenerali aliyekuwa akishangiliwa na wahudhuriaji. 

“Iwapo mawaziri wa zamani wamechukuliwa hatua na kupelekwa mahakamani kwa kusababisha hasara, Mheshimiwa Kikwete anastahili kupelekwa mahakamani kwa kusababisha hasara kwa Serikali na kuzima matumaini ya wananchi na kuachwa wanarandaranda wasijue wafanye nini na baadaye inaweza kutuletea machafuko, kama hatukuweza kutengeneza Katiba ambayo itatuwekea mustakbali wa Watanzania,” alisema. 

Jenerali alisema suala la Katiba limekwama na limekwamishwa kwa makusudi kabisa. 

Kuhusu Mwalimu Nyerere, Jenerali alisema asingekuwa anazungumzwa kwa sifa nyingi kama sasa, iwapo asingechukua uamuzi wa mwaka 1992 wa kuruhusu mfumo wa vyama vingi, licha ya kwamba waliokuwa wameukubali ni asilimia 20 ya Watanzania. 

Kuhusu Rais John Magufuli, Jenerali alisema pamoja na sifa anazopewa sasa za utendaji wake, akitazamwa kwa uwanda mpana, nchi imerudi nyuma kwa miaka 50 kwa masuala ya demokrasia. 

Akifafanua namna nchi ilivyorudi nyuma, alisema, “Kwa kufinya uhuru wa kujieleza na hususan kwa kufinya uhuru wa wawakilishi wa wananchi ndani ya Bunge.” 

Baadaye, Rais mstaafu, Benjamin Mkapa ambaye alikuwa mgeni rasmi katika tamasha hilo alifafanua kauli ya Jenerali kwa kusema yeye (Mkapa) hakuwa mshauri wa Rais, bali Jaji Warioba alimfuata atoe ushauri na hakuwa kwenye ngazi yoyote ya uamuzi. 

“Kwenye chama changu sikuwemo na kwenye Serikali sikuwemo. Siwezi kulizunguzumzia hilo na waandishi wanapenda nitoe maoni,”alisema Mkapa. 

Alisema ipo haja ya kujiuliza kwa nini Katiba hiyo ilikwama na hadi sasa hajasikia uchambuzi wa kina kuhusu jambo hilo.

“Kuna haja ya kuwa na mjadala mkubwa lakini siyo kulaumiana tu. Siyo kudai tu. Kuwezesha uhuru wa kuzungumza ni jambo moja na kutumia uhuru huo ni kujadili, kuchambua na kupima na kufanya uamuzi sahihi kitu kingine kabisa,”alisema Mkapa. 

Alisisitiza kuwa badala ya kumlaumu mtu mmoja mmoja, mjadala mpana wa kitaifa unahitajika ili kujua kilichosababisha Taifa kukosa Katiba Mpya. 

“Hakuna anayeandika ni wapi tulipokwama, tunalaumu na kumjadili mtu, wengine wanasema Katiba imekwamishwa na watu wachache kwa sababu za kimaslahi…tunapaswa kuwa na mjadala wa kina kujua ni wapi tulipokwama,” alisema Mkapa. 

Aidha, Jenerali aliwananga viongozi wastaafu akisema amebaini sasa kuwa kwa bahati mbaya wanapata busara baada ya kuacha nafasi za uongozi. 

Alisema ili kuwa na busara wakati mtu akiwa madarakani, anatakiwa awasikilize wale anaowaongoza na njia moja ya kufanya hivyo ni kuwapa Katiba ambayo ndiyo mwongozo utakaosimamia mustakabali wao. 

Awali, akiwasilisha mada katika tamasha hilo, Mkapa alisema si kana kwamba Mwalimu Nyerere hakupenda kampuni binafsi zije kuwekeza nchini bali alipenda biashara na uwekezaji vifanyike kwa haki, usawa na kuchangia maendeleo ya nchi. 

Kuhusu sukari, Mkapa ambaye alijitetea kwa kuanzisha sera ya ubinafsishaji, alisema wakati anaingia madarakani, viwanda vya sukari vikiwamo Kilombero na Mtibwa vilikuwa havizalishi kabisa au kuzalisha kidogo, hivyo kulikuwa na tatizo la sukari. 

Alisema baada ya ubinafsishaji, sukari ilianza kuzalishwa kwa wingi lakini akahoji ni nini hakikufanyika hadi nchi ikafikia mahali ilipo sasa.

Ugawaji mikoa 
Akichangia mjadala huo, mhadhiri mwandamizi wa Taasisi ya Taaluma za Kiswahili (Tataki) ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Martha Qorro alisema Serikali imeendelea kuongeza idadi ya mikoa, jambo ambalo linazidi kuwagawa wananchi. 

Pamoja na kuathiri umoja wa kitaifa, mhadhiri huyo alikuwa na maoni kuwa, fedha nyingi kwa sasa zinatumika kuendesha mikoa inayoongezwa badala ya kuleta maendeleo kwa wananchi. 

Hata hivyo, Mkapa alisema wakati wa uongozi wake aliongeza mkoa mmoja tu wa Manyara, ambao aliumega kutoka Arusha baada ya kuona uhitaji na kufanya vikao. 

Rais huyo mstaafu alisema suala la kuzingatia wakati wa ugawaji wa mikoa ni kutowagawa wananchi kwa misingi ya ukabila na udini. 

Mstaafu huyo aliyeiongoza nchi kipindi cha mwaka 1995-2005, alisema suala la kuangalia ni mahitaji ya watu ndiyo maana alikaa na viongozi wa maeneo yote hayo na hatimaye kufanikiwa kuigawa Arusha. 

Alisema Watanzania wengi wamekuwa na desturi ya kutumia muda mwingi katika kuilaumu Serikali badala ya kufanya kazi kwa maendeleo ya nchi. 

“Watanzania tunatakiwa tufanye kazi kwa bidii ili tuifikishe nchi yetu kwenye maendeleo na si kutumia muda mwingi katika kuilaumu Serikali,” alisema Mkapa. 


Maalim Seif Awahutubia Wamarekani Kuhusu Sakata Zima la Zanzibar

Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharrif Hamad amesema vitendo vya unyanyasaji wapinzani vinavyoendelea nchini ni maradhi yanayokikumba chama tawala. 

Maalim Seif aliyasema hayo alipokuwa akihutubia mkutano uliondaliwa na Kituo cha Elimu cha Kimkakati cha Kimataifa cha Marekani (CSIS) juzi, uliofanyika Washington DC nchini Marekani. 

Akizungumzia kukandamizwa kwa wapinzani nchini, Maalim Seif alitoa mfano wa yeye kuhojiwa na polisi 11 kwa saa tatu na kijana aliyehukumiwa kifungo cha miaka mitatu au kulipa faini ya Sh7 milioni kwa kumkosoa Rais John Magufuli kwenye ukurasa wa facebook. 

Kadhalika alitoa mfano wa viongozi wa Chadema kuhojiwa polisi na baadhi kuwekwa rumande kwa saa kadhaa huku kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo naye akihojiwa kwa kufanya mkutano. 

“Tunashuhudia mmomonyoko wa hali ya juu wa demokrasia sasa hivi… na hali hii itazidi miezi michache ijayo,” alisema. 

Alisema wapinzani wanakandamizwa zaidi upande wa Zanzibar, na kusema kuwa CUF inataka ufafanuzi wa Muungano na wala si kuufuta.

Kiongozi huyo wa CUF alimlaumu Rais John Magufuli na kusema licha ya kuwa nchi za nje zinamuona anafanya vyema katika kupambana na rushwa, lakini Wazanzibari hawana furaha na uongozi wake. 

“Kuna mitazamo tofauti hasa kwa walio nje ya Tanzania kwamba anapambana na rushwa, lakini kama kiongozi wa nchi, ameshindwa kufanya majukumu yake kuhusu Zanzibar,” alisema

Alisema mara zote Rais Magufuli anapoulizwa kuhusu suala la Zanzibar, husema hawezi kuchukua hatua.

“Wazanzibari wanachokitaka ni kuona Rais Magufuli anawajibika kama kiongozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” alisema Maalim Seif ambaye katika mkutano huo, aliambatana na mkurugenzi wa Mambo ya Nje wa CUF, Ismail Jussa Ladhu na katibu wake, Issa Kheri Hussein. 

Pamoja na mambo mengine, Maalim Seif alisema chama chake kipo tayari kufanya uchaguzi mwingine, endapo utasimamiwa na taasisi za kimataifa zisizofungamana na upande wowote. 

Alisema wakati wakisubiri hilo, wafuasi wa chama hicho wanaendelea kufanya mgomo baridi usio na nia ya vurugu ili kuonyesha kuwa mambo hayawezi kwenda kama kawaida. 

Akijibu swali la mmoja wa waliohudhuria mkutano huo kuhusu kutuhumiwa kuuvunja Muungano endapo atakuwa Rais wa Zanzibar, Maalim alisema chama tawala kimekuwa kikivibatiza vyama vya upinzani majina ya uongo ili kuvibomoa.

 “Kuna wakati walikiita CUF kuwa ni chama cha Kiislamu, lakini hilo si kweli, tumenyang’anywa ushindi zaidi ya mara tano na wala hatujaleta fujo,” alisema. 

Katika mkutano huo uliohudhuriwa pia na Rais Alassane Ouattara wa Ivory Coast, Maalim alielezea jinsi uchaguzi wa Oktoba 25, mwaka jana ulivyofutwa na kusema kuwa CUF imekuwa ikinyang’anywa ushindi tangu mfumo wa uchaguzi wa vyama vingi uanze mwaka 1995. 

“Tumefanya chaguzi tano, 1995, 2000, 2005, 2010 na 2015 katika chaguzi zote hizi, watu wa Zanzibar waliichagua CUF kuongoza Serikali. Lakini CUF imenyimwa kushika madaraka,” alisema Maalim na kuongeza:

 “Kuna harufu ya hatari, kwa miaka yote hiyo tumejitahidi kuwatuliza wafuasi wetu, tumeangalia namna ya kuzungumza na wenzetu ili waheshimu maamuzi ya watu, lakini hawasikii.” 

Alisema uchaguzi wa mwaka jana ulifanyika kwa uhuru na haki na matokeo yalionyesha kuwa CUF kimeshinda, lakini polisi waliizingira Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) na baadaye Mwenyekiti wa tume hiyo, Jecha Salim Jecha akayafuta matokeo hayo. 

Alisema hata Umoja wa Ulaya (EU) walitoa ripoti yao wiki mbili zilizopita, iliyoonyesha kuwa ZEC haikuwa na mamlaka ya kufuta matokeo hayo. 

“Nilijaribu kuwasiliana na Dk Ali Mohamed Shein , lakini hakutaka kupokea simu yangu, lakini baadaye nilimuandikia barua nikitaka mazungumzo naye, alikubali kwa masharti kuwa wawepo watu wengine.”alisema na kuongeza: “Tukakubaliana tufanye mazungumzo, lakini wawepo viongozi wakubwa, wakati tukiendelea na mazungumzo, Jecha alitangaza kuwa uchaguzi utarudiwa Machi 20.” 

Maalim Seif alitaja athari za kufutwa kwa uchaguzi huo kuwa ni pamoja na kuvunja maridhiano ya kisiasa ya Zanzibar na Maamuzi ya Wazanzibari wengi walioamua nchi yao iongozwe kwa Mfumo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK).

Alitaja athari nyingine kuwa ni kuwarudisha nyuma watu wa visiwa vya Unguja na Pemba, kuibuka kwa siasa za chuki, migogoro na kubaguana. 

“Hayo ni pamoja na kudhoofika kwa sekta za uchumi, biashara, ukosefu wa ajira na maendeleo kwa jumla, na siyo kwa Zanzibar pekee bali kwa Jamhuri yote ya Muungano wa Tanzania, hasa iwapo Mataifa yataitenga na kulinyima Taifa misaada, hali ambayo haiwezi kuepukika”. alisema 

Akieleza msimamo wa waandaaji wa mkutano huo, uliojumuisha marais mbalimbali wastaafu wa Marekani na Ulaya, Mkurugenzi Mkuu wa NDI, Peter Craig aliwataka viongozi wa kisiasa wa nchi nyingine za Afrika kuiga mwenendo wa Maalim Seif. 

“Tunaomba watu wengine wenye migogoro ya aina hii waige mfano huu wa Seif Sharif Hamad na sisi tutakuwa pamoja nao mpaka haki itendeke na ipatikane na tukianzia na Zanzibar,” alisema

Lowassa Amwandikia Waraka Mzito Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Ernest Mangu


WAZIRI Mkuu wa zamani na aliyekuwa mgombea urais wa Chadema kwa mwamvuli wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Edward Lowassa, amemwandikia barua Mkuu wa Jeshi la Polisi   (IGP), Ernest Mangu.

Katika barua hiyo, Lowassa  amehoji hatua ya Jeshi la Polisi kupiga marufuku mikutano na maandamano kwa vyama vya siasa vya upinzani nchini.

Katika barua yake hiyo ya jana, Lowassa  alisema amelazimika kuchukua hatua hiyo kwa vile  wakati agizo hilo la  kupiga marufuku   mikutano inatolewa, alikuwa nje ya nchi ingawa alifikisha ujumbe na Watanzania wenye nia njema wa ndani na nje kuhusu hatua hiyo ya polisi.

“Kwanza niwie radhi kwamba nimelazimika kwa nafasi yako na yangu, kukiuka taratibu za itifaki hata nikalazimika kuandika waraka huu kwako.

“Ninafanya hivyo si kwa sababu yoyote, bali kwa sababu tu jambo au mambo yaliyonisukuma kukufikishia ujumbe huu yana uzito mkubwa na kimsingi yanaweza kuathiri mustakabali mwema wa taifa.

“IGP, siyo desturi yangu kuandika waraka wa namna hii mtandaoni au kupitia vyombo vya habari, ingawa safari hii nimelazimika kufanya hivyo   kuweka rekodi sahihi,   na kukosoa sababu ulizotoa kuwa nyuma ya agizo lako hilo,” alisema Lowassa.

Alisema wakati akiwa anatafakari kwa mshangao agizo hilo na baada ya kurejea nchini, alipigwa na butwaa zaidi baada ya kusikia Jeshi la Polisi katika mikoa ya Kanda ya Ziwa, limewazuia viongozi wao taifa wa vyama vya siasa kufanya mikutano ya hadhara.

“Agizo hilo lilifuatiwa na tukio la kukamatwa, kushikiliwa na kuhojiwa kwa viongozi hao, akiwamo Mwenyekiti wetu, Freeman Mbowe huko Mwanza hivi majuzi.

“Katika matukio hayo yote, polisi mnadai kuwa na taarifa za intelijensia ambazo zinaonyesha kuwapo  uwezekano wa kutokea  vurugu kwenye mikutano hiyo ya hadhara ya vyama vya siasa,” alisema.

Lowassa  alisema madai hayo ya polisi hata IGP Mangu, aliwahi  kuyatoa awali kutokana na sababu wanazozijua wao wenyewe kama njia ya kuminya haki za msingi za katiba za vyama vya siasa kujumuika na kutimiza majukumu yao ya siasa.

“Si hivyo tu, uzoefu wa historia unakinzana na kwenda kinyume kabisa na madai hayo, kwa sababu  yako matukio mengi ambayo yamethibitisha kwamba mijumuiko ya wanasiasa wa vyama vya upinzani, yakiwamo maandamano na hata mikutano, imekuwa ikifanyika kwa amani.

“Iko mifano mingi inayoonyesha kwamba  tumefanya shughuli mbalimbali za siasa kwa maana ya maandamano na mikutano yahadhara kwa amani na pasipo kuwapo hata   ulinzi wa polisi.

“…Mifano ya namna hiyo ndiyo inayosababisha baadhi yetu si tu tupingane na maagizo yanayotoa mwelekeo wa kukandamizwa   uhuru wa  katiba wa vyama vya siasa vya upinzani kujumuika, bali kwenda mbali zaidi na kutilia shaka hata maagizo hayo na kuyaona kuwa na misukumo iliyojificha nyuma ya kichaka cha ‘sababu za intelejensia,”alisema.

Alisema anaandika barua hiyo aliyoiita waraka kwa mkuu huyo wa polisi kwa dhati   kwamba,  kilichotokea Kenya hivi karibuni ambako mahakama ilitupilia mbali maagizo ya namna hiyo ya polisi kujaribu kuzuia haki ya katiba ya vyama vya upinzani kuandamana ndicho kinachoelekea kutokea hapa nchini.

Maalim Seif ampiga stop Prof. Lipumba

                                     


Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharrif Hamad (kulia) akiwa na Aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahim Lipumba
JUHUDI za Prof. Ibrahim Lipumba, kurejea katika nafasi yake ya uenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), zimegonga mwamba, Maalim Seif Sharif Hamad, katibu mkuu wa chama hicho taifa, “amekataa kubariki” hatua za Lipumba kurejea katika nafasi hiyo; hata kuwania nafasi nyingine yoyote katika chama.
Maalim amekaririwa akisema hayo wakati wa kujibu swali la mmoja wa waandishi wa habari wa Tanzania anayefanya kazi zake nchini Marekani.
Alisema, Prof. Lipumba “alijiuzulu mwenyewe miezi minane iliyopita. Hakulazimishwa; yeye mwenyewe alionyesha nia ya kutaka kujiuzulu.”
Anasema, “watu wengi, wakiwamo wazee na mashekhe, walimfuata kumuambia tafadhali usijiuzulu; lakini akaendelea na azma yake. Akajiuzulu.”
Maalim Seif anasema, Prof. Lipumba hakushindikizwa na mtu kujiuzulu, barua yake aliipokea na kuipeleka kwenye Baraza Kuu la Uongozi (BKU) ambako wajumbe kwa kauli moja, wakaridhia kuachia ngazi.
“Baraza Kuu wakaipokea taarifa ile, wakachagua Kamati ya Uongozi ya muda ya kuongoza chama mpaka hapo atakapo patikana mwenyekiti mpya. Kamati ile bado ipo na Maalim Seif hana uwezo wa kuiondoa.”
Akiongea kwa sauti ya ukali, Maalim Seif alisema, “Kamati ile imewekwa na Baraza Kuu la uongozi la taifa. Haiwezi kuondolewa na Maalim Seif na huwezi kuwa na uongozi juu ya uongozi.”
Msimamo wa Maalim Seif unashahabiana na ule wa Naibu Katibu mkuu wa CUF Visiwani, Nassor Ahmed Mazrui, anayesema kuwa Prof. Hana nafasi katika chama chake.”
Anasema, “Prof. Lipumba hana nia njema. Anataka kuja kuiharibu CUF. Anataka kuharibu mipango yetu.”
Akiwa anahaha kurejea katika nafasi yake ya uenyekiti wa CUF, Prof. Lipumba amesema ameamua kurejea tena katika nafasi yake kutokana na “kuombwa na makundi ya wanachama na viongozi wa dini…”
Amesema ametafakari kwa kina maombi hayo huku akizingatia hali halisi ya siasa ya Visiwani ambayo kwa sasa si shwari.
Uamuzi huo anasema, ameuchukua kwa kuzingatia Ibara ya 117 ya katiba ya CUF inayoelezea kwa undani jinsi kiongozi anavyoweza kujiuzulu na kurejea tena ndani ya chama hicho.
Taarifa zinasema juhudi za Prof. Lipumba kurudi kileleni zinalenga kuvunja nguvu za Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) zilizodhihirika wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka jana.
Hata hivyo, habari kutoka ndani ya CUF zinasema, shinikizo la kutaka Prof. Lipumba kurejea katika nafasi yake bila kufanyika uchaguzi, linatokana na baadhi ya wapambe wake kunusa kuwa kiongozi huyo hawezi kushinda katika uchaguzi wa ndani ya chama.
“Baada ya kuona Prof. Lipumba hawezi kushinda uchaguzi, viongozi wake wawili (majina tunayo), wakatengeneza mkakati ili arejeshwe katika nafasi yake,” ameeleza kiongozi mmoja wa chama hicho aliyeko Buguruni, Dar es Salaam.
Amesema, “lakini nataka nikuambie, Prof. Lipumba hana tena nafasi ndani ya CUF. Kuruhusu Prof. Lipumba kurejea CUF akiwa mwenyekiti ni kutaka kuangamiza Ukawa. Nasi tunajua kuwa Ukawa umeumiza sana CCM. Hatutakubali.”
Prof. Lipumba alijivua nafasi ya mwenyekiti Agosti mwaka jana, katikati ya vuguvugu la uchaguzi mkuu, huku mgombea wa Ukawa, Edward Lowassa akitikisa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kilichosimamisha John Pombe Magufuli.

Basi la Kampuni ya Tahmeed Lateketea Kwa Moto barabara ya Chalinze- Segera


Basi la Abiria la Kampuni ya TAHMEED linalofanya safari zake kati ya Tanga- Dar es Salaam, limeteketea kwa moto katika barabara ya Chalinze- Segera.

Taarifa kutoka eneo la tukio zinaeleza kuwa hakuna mtu aliyefariki wala kujeruhiwa kutokana na ajali hiyo lakini mizigo ya abiri ndiyo imeteteketea ndani ya basi hilo.

Ajali imetokea wakati basi hilo likiwa limesimama baada ya Abiria mmoja kuomba Msaada akajisaidie (kuchimba dawa) na ndipo abiria waliokuwamo ndani ya gari alianza kusikia harufu ya moshi wa tairi linaloungua na ndipo wakatoka nje ya gari na muda mfupi gari lote likashika moto.

May 25, 2016

Wolper aeleza yaliyomkuta mpaka akampiga chini Mkongo, adai Mkongo alimpiga picha za uchi ili asimuache

Msanii wa filamu Jacqueline Wolper amefunguka na kuzungumzia sababu ya kuachana na aliyekuwa mpenzi wake ambaye alimvalisha pete ya uchumba pamoja na kwenda kwao kwa ajili ya maandalizi ya kumtolea mahari ili amuoe.
wolp2
Wopler na mpenzi wake wa zamani
Muigizaji huyo ambaye amekiri kutoka kimapenzi na Harmonize wa WCB, amekiambia kipindi cha Take One cha Clouds TV kuwa, Mkongo huyo ambaye alimvalisha pete ya uchumba, alikuwa ana mke pamoja na mtoto na pia alimfanyia kitendo cha kinyama cha kumrekodi picha za uchi ili asimuche.
“Mimemvumilia kumkuta na picha zangu za uchi, video zangu za uchi,” alisema Wopler huku akilia.
“Nikiongelea nimezionaje nitakuwa namvunjia heshima, kwa sababu kuna kitu kibaya alikifanya. Kuna matatizo ambayo yalitokea nikawa namkwepa, niligundua ana matatizo mengi nikawa namkwepa, nilikuwa na stress nikawa nalewa sana, nalewa mpaka nazima. Sasa siku ambayo nimelewa sana mpaka nimezima akaambiwa nilipo, nilikuwa nipo mimi, dada yangu mmoja pamoja na mdogo wangu mmoja nimelewa chakari, nimechanyikiwa siyo mimi. So kilichotokea akaja akanichukua, akanipeleka nyumbani kwake, akanivua nguo zote, nilikaa kwenye kitanda chake, nipo uchi wa mnyama, yaani sijui chochote kinachofanyika, akarekodi video na kunipiga picha,” aliongeza Wolper.
c79e987f-01b7-4137-abf1-e66acf4f90cf
Harmonize na Wopler ndani ya mahaba
Muigizaji huyo amesema baada ya kugundua kuwa mpenzi wake huyo alimpiga picha za uchi, alimuomba azifute lakini akawa anamtishia kuzisambaza kama akimuacha.
“Kitu cha ajabu ambacho kilikuja kunishangaza wiki mbili zilizopita, aliniambia kitu nitachokifanya baada ya kugundua kwake sipo vile kama zamani, akaniambia kitu nitakacho kufanya, watanzania watafunga macho, meseji zake zote ninazo na nimemkabidhi mwanasheria wangu na nimeshaandikisha kila kitu, akaniambia kitu nitakacho kifanya watanzania hawata amini, nikamwambia najua ulinichua video za uchi, akaniambia kumbe ndiyo hicho tu unachokifahamu, sasa sijajua ni nini sijawahi kufanya uhalifu kwake wala nini,” alisema Wolper.
Pia Wolper amedai alipelekwa Afrika Kusini ili akasome lakini akaishia kudanganywa na kukaa Afrika Kusini kwa miezi mitatu bila chochote na kuamua kurudi zake Dar es salaam.

Magufuli afumua TCU, St. Joseph yaponza wengi

Dk. John Magufuli, Rais wa Tanania
RAIS John Magufuli amevunja Kamisheni  ya Tume vya Vyuo Vikuu (TCU) na kuwasimamisha kazi watendaji wakuu wa tume hiyo baada ya kubainika kudahili wanafunzi wasio na sifa na kuwapa mikopo, Pia serikali imetangaza kufanyika kwa udahili upya Vyuo Vikuu vyote nchi nzima ili kuwaondoa vyuoni wanafunzi wote wasio na sifa sambamba na kutangaza vita kali kwa wanafunzi hewa wanaopata mikopo ya elimu ya juu.

Hayo yamebainishwa leo na Prof. Joyce Ndalichako Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia alipozungumza na waandishi wa habali juu ya kuvunjwa kwa Kamishina ya TCU.
Amesema, kwa idhini aliyopewa na rais anawasimamisha kazi mara moja watendaji hao wa Kamisheni ya Tume ya Vyuo Vikuu.
Prof. Ndalichako amewataja waliosimamishwa kazi kuwa ni Prof. Yunus Mgaya, Katibu Mtendaji wa TCU kwa kushindwa kusimamia kazi za TCU akiwa kama mtendaji mkuu wa taasisi hiyo.

Pia, Dk. Savius Maronga, Mkurugenzi wa Udhibiti na Ubora kwa kushindwa kutekeleza wajibu wake wa kusimamia ubora na ithibati ya Vyuo Vikuu.
Amesema Rose Kiishweko, Mkurugenzi wa Udahili amesimamishwa kwa kushindwa kusimamia udahili wa wanafunzi na kupelekea kudahiliwa wanafunzi wasio na sifa, na mwingine aliyesimamishwa ni Kimboka Istambuli  ambaye alikuwa Kaimu Mkurugenzi wa  Udahili na Nyaraka.

Mbali na hilo Prof. Ndalichako amesema, ili shughuli za TCU ziendelee, Prof. Eliuter Mwageni ameteuliwa kukaimu nafasi ya katibu mtendaji  na kabla ya uteuzi wa kukaimu nahfasi hiyo Prof. Mwageni alikuwa Naibu Makamu Mkuu (Utawala na Fedha) wa Chuo Kikuu cha Ardhi.

 Aidha ameteuliwa Dk. Kokubelwa Mollel ambaye atakaimu nafasi ya ukurugenzi wa udahili na nyaraka na kabla ya uteuzi  wa kukaimu nafasi hiyo Dk. Kokubelwa  alikuwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Amesema kwa muda mrefu kumekuwa na taarifa za wanafunzi wa Chuo Kikuu cha St. Joseph wanaodahiliwa kutokuwa na sifa.
Waziri amesema, kutokana na hilo serikali imeamua kutoa tamko baada ya ukaguzi kufanyika katika chuo hicho katika kampasi za Arusha na Songea na kubaini kuwepo kwa upungufu mkubwa katika utoaji wa elimu isiyokuwa na kiwango.

Amesema, walibaini kuwepo kwa wanafunzi 489 ambao wapo katika vyuo hivyo ambao hawakidhi viwango na hawana sifa za kusoma Chuo Kikuu.

Amesema kibaya zaidi ni kuwepo kwa wanafunzi ambao ni wa kidato cha nne waliofaulu Daraja la Nne huku wengine wakiwa na pointi 32 lakini wakidahiliwa kusomea shahada ya kwanza .
“Mwanafunzi wa Kidato cha Nne anasoma digrii ya Sayansi, huku mtu huyo akiwa sekondari kasoma mkondo wa biashara lakini kadahiliwa asomee Sayansi na analipiwa mkopo na TCU.
“Si tu hana sifa ya kusoma Chuo Kikuu, hana hata sifa ya kuwa na cheti cha ualimu kwa maana hiyo mtu wa aina hiyo  hafai hata kuwa na cheti cha ualimu hatuwezi kukubali mtu wa jinsi hiyo akasomee digrii,” amesema.

Prof. Ndalichako amesema rais amekuwa akihangaika kutafuta fedha kwa ajili ya mikopo ya elimu ya juu lakini cha kusikitisha kuna wanafunzi waliofaulu vizuri Kidato cha Sita wanakosa mikopo ila wale waliofeli wanapata mikopo hiyo.
“Divisheni four pointi 34 yuko Chuo Kikuu hata ualimu simkubali mtu wa namna hiyo,” amesema.

Amesema, baada ya serikali kufunga chuo hicho wanafunzi hao walihamishiwa vyuo mvingine lakini hata huko walikopelekwa uwezo wao umeonekana kuwa ni mdogo hali iliyolazimu kuwarudisha madarasa ya nyuma.
‘Wanafunzi waliotoka St. Joseph na kupelekwa Chuo Kikuu cha Dodoma uwezo wao umeonekana kuwa ni mdogo, ambapo wanafunzi wa mwaka wa pili na wa kwanza wamerudishwa nyuma muhula moja huku wale wa mwaka wa tatu wamerudishwa nyuma mwaka moja” amesema.

 Amesema, wale wa St. Joseph Tawi la Songea waliopelekwa Chuo Kikuu cha Kilimo Morogoro (SUA) waliokuwa wakisoma mwaka wa nne wamerudishwa mwaka wa tatu na wametengewa vipindi vya ziada ili kurekebisha upungufu huo, na hata wale waliopelekwa vyuo vingine vya Ruaha, Mkwawa wameonekana kuwa na upungufu pia.
 “Kibaya zaidi hao wanafunzi walikuwa wanapata mikopo, Division four anapata mkopo haki iko wapi, tulipoona jambo hili si sawa, tulichukua hatua tukaieleza bodi ya TCU kusimamisha kazi waliohusika lakini hilo halikufanyika,” amesema.

Kufuatia kuwepo kwa matatizo hayo Prof. Ndalichako ametangaza vita kwa vyuo mbalimbali ambavyo vina watu ambao wanadahili wanafunzi wasio na sifa.
Kuhusu wanafunzi ambao hawakuwa na sifa lakini walikuwa wakisoma chuo kikuu hicho amesema licha ya kuwa wamepoteza muda wao mwingi lakini watalazimika kurejesha mikopo hiyo.
“Wale wote ambao walipata mikopo bila kuwa na sifa watarejesha mikopo hiyo na hakuna njia yoyote ya kuwasaidia bali wanatakiwa kuendelea kuangalia ni jinsi gani ya kujiendeleza,” amesema.